0
UPANDE wa Jamhuri katika kesi
inayowakabili wafuasi watatu wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) umedai mahakamani kwamba washtakiwa hao walikiuka amri halali ya Jeshi la Polisi baada ya kuvuka kizuizi kilichowekwa eneo la Makao Makuu ya jeshi hilo.

Kadhalika, washtakiwa hao Ngaiza
Kamugisha (28) dereva, mkazi wa
Vingunguti, Benito Mwapinga (30) Fundi
nguo mkazi wa Mtoni kwa Azizi Ally na
Eliasante Bugeji (51) Mhasibu wa CCBRT
mkazi wa Komakoma Kinondoni, Dar es
Salaam, wanadaiwa kukiuka amri halali
iliyotolewa na Inspekta Zuhura ya
kuwataka kutoweka eneo la ofisi hiyo.

Madai hayo yametolewa leo na Wakili wa Serikali Mkuu, Bernad Kongola wakati akiwasomea maelezo ya awali mbele ya Hakimu Mkazi Frank Moshi.

Kongola alidai kuwa Septemba 18, mwaka huu katika makao makuu ya jeshi la Polisi, washtakiwa walizuiliwa kuingia eneo hilo lakini walikiuka amri hiyo na kuingia kwa jinai.

Ilidaiwa kuwa mshtakiwa wa tatu, alitoa
lugha chafu na matusi kwa Inspekta
Zuhura iliyosababisha uvunjifu wa amani.
Washtakiwa walikana maelezo hayo.
Hakimu Moshi alisema kesi hiyo itasikilizwa Septemba 22 na 23, mwaka huu ushahidi wa upande wa Jamhuri.

Katika kesi ya msingi, ilidaiwa kuwa
Septemba 18,mwaka huu, washtakiwa
waliingia kinyume na sheria ndani ya
Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kwa hali ya fujo.

Alidai tarehe na siku ya tukio la kwanza
washtakiwa walikataa kutii amri ya halali
ya kutawanyika eneo la makao hayo
iliyotolewa na Inspeta Zuhura, ambaye
alitoa amri hiyo baada ya kuruhusiwa na
viongozi wake.

Chapisha Maoni

 
Top