0
Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi wa
Bunge Maalu la Katiba, Mhe. Andrew
Chenge akiwasilisha Rasimu
iliyopendekezwa ndani ya bunge hilo leo 24 Septemba, 2014 mjini Dodoma.





Mambo yameiva, na hii hapa ndiyo
Rasimu ya Tatu ya Katiba, ambayo
inapendekezwa na Bunge
Maalum. Vipengele vingi
vimebadilishwa. Haya hapa ni mambo ya
Muungano:
Mambo ya Muungano
1. Katiba na Mamlaka ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
2. Ulinzi na usalama wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
3. Usalama na usafiri wa anga.
4. Uraia na uhamiaji.
5. Jeshi la Polisi.
6. Sarafu na Benki Kuu.
7. Kodi ya Mapato inayolipwa na watu
binafsi na Mashirika, ushuru wa forodha
na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa
nchini Tanzania na zinazosimamiwa na
Idara ya Forodha.
8. Mambo ya nje.
9. Usajili wa vyama vya siasa.
10. Mahakama ya Juu na Mahakama ya
Rufani.
11. Elimu ya Juu.
12. Baraza la Taifa la Mitihani na mambo
yote yanayohusika na kazi za Baraza hilo.
13. Utabiri wa hali ya hewa.
14. Utumishi katika Serikali ya Jamhuri
ya Muungano.

Chapisha Maoni

 
Top