0

MANCHESTER United ya Louis Van Gaal
imeanza ligi. Hivyo ndivyo unavyoweza
kusema kufuatia Mashetani hao Wekundu kuifumua mabao 4-0 QPR katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Old Trafford.

Winga Muargentina, Angel di Maria ndiye
aliyefungua pati la mabao United leo baada ya kufunga bao la kwanza kwa mpira wa adhabu
dakika ya 24.



Ander Herrera akaifungia Manchester United bao la pili dakika ya 35 kabla ya Wayne Rooney kufunga la tatu dakika ya 44 na Juan Mata akapiga la nne dakika ya 58.

Radamel Falcao alianzia benchi, akaingia dakika ya 67 kuchukua nafasi ya Juan Mata.

Kikosi cha Man Utd kilikuwa: De Gea, Rafael/ Valencia dk67, Evans, Rojo, Blackett, Blind, Herrera, Mata, Di Maria/Januzaj dk82, Rooney, Van Persie


QPR: Green, Isla, Ferdinand, Caulker, Hill,
Sandro, Kranjcar, Fer, Phillips, Austin, Hoilett.

Chapisha Maoni

 
Top