
Santos ‘Jaja’ alifunga mabao mawili katika mchezo huo, wakati Simon Msuva alifunga la tatu, yote kipindi cha pili.
Dakika 45 za kwanza zilimalizika timu hizo zikiwa hazijafungana na timu zote
zilishambuliana kwa zamu.
Azam ilitawala mchezo dakika 30 za
mwanzoni, lakini Yanga ilichangamka baada ya kocha Marcio Maximo kumpumzishachipukizi Said ‘Kizota’ Juma na kumuingiza Hassan Dilunga aliyekwenda kufanya kazi
nzuri.
Chapisha Maoni