0
Muigizaji maarufu wa filamu nchini Happy Nyatawe ambaye pia ni mfanyabiashara amewaasa
wanawake wenzake kuacha kuwa magolikipa kwa wanaume na pia kuacha umbeya na badala yake
wajikite katika kazi ili kujiletea maendeleo.

Akizungumza na Mpekuaji, Happy amesema: "Nashangaa wanawake ambao mpaka karne hii
wanategemea wanaume Kwanini siku moja na wewe mpenzi wako au mumeo asifurahie msaada
toka kwako ?

"Wanawake tunaweza kataa u-golikipa na vikao vya umbeya mitaani, u-busy unaepusha mambo mengi sana .Tuwe bize kusaka pesa na si kusuta watu.
"Mimi mbali na biashara yangu muda mwingi napenda kupumzika nyumbani na kuangalia movie, yaani kazi za wenzangu na endapo
itatokea msiba au sherehe hujumuika na
wenzangu lakini naogopa sana kusutwa ndo maana sipend vigenge"


Chapisha Maoni

 
Top