Muigizaji maarufu wa filamu Tanzania 'Johari' Blandina Chagula amsema kuwa kuandikwa vibaya na uzushi kwa mambo yanayodhalilisha ndiyo
mambo yanayokwaza na kukatisha tamaa katika uigizaji.
Akizungumza na gazeti moja la kila siku lisilo la udaku Johari aliweka wazi kuwa star wa filamu nchini anahitajika kuwa na moyo mgumu kwa kuwa uzushi na mambo mbalimbali ya
kusingiziwa huchangia kwa kiasi kikubwa kuwaondoa kwenye tasnia hiyo waigizaji wengi wakubwa.
Johari ameyasema hayo huku baadhi ya wasanii wakiyalalamikia baadhi ya magazeti ya udaku kwa madai ya kuwaandika kwa habari za uongo na
wakati mwingine hutokea pale msanii anapokuwa hakubaliani na matakwa yao katika kitu flani na kuishia kuandikwa kwa habari za kumchafua.
Chapisha Maoni