Staa wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’, amefunguka kuwa kwa sasa hana mpenzi wala hajapata mtu wa kumuoa ila anataka kuolewa na mzee atakayeweza kumlea.
Akizugumza na wanahabari wetu kwenye mgahawa wake wa Ray C uliopo Mwananyamala, Dar, mwanadada huyo alisema yeye kama mwanamke anatamani kuolewa na kupata mtoto
si na ‘serengeti boy’ bali mzee.
Aliendelea kutiririka kwamba akikosa wa kumuoa atatafuta mwanaume atakayemlipa kwa ajili ya kuzaa naye tu lakini ni pale atakapokuwa anaweza
kulea mwenyewe.
Ray C aliongeza kuwa, kwa sasa anatafuta wadhamini kwa ajili ya kuendesha taasisi yake ya Ray C Foundation kwani amefanikiwa kuwasaidia watu wengi kupata kazi na kuachana na dawa za
kulevya.
Chapisha Maoni