Ni leo asubuhi ndipo taarifa za msiba wa aliyekua msanii wa TMK Wanaume Family aliyekua akijulikana kama YP.
Kwa mujibu wa maelezo aliyetoa Said Fella ambaye ndio kiongozi wa
wanaume Family ni kua marehemu alianza kuumwa tangu mwezi wa nane mwaka jana. Na afya yake ilikua
ikiendelea vizuri mpaka siku ya jumapili
alipozidiwa na kukimbizwa hospitali ya Temeke ambapo usiku wa kuamkia leo ndipo mauti yalipomkuta.
Tulipomuuliza kuhusu kazi alizoziacha marehemu Said alisemakua ndio kuna nyimbo moja ambayo imewakutanisha TMK Wanaume Family na Tip Top
ambapo marehemu alihusika katika kumba wimbo huo. Kuhusu utaratibu wa mazishi Said amesema kua wamekubaliana kua yatafanyika kesho.
Chapisha Maoni