0
Mkazi wa Buguruni, Rukia Nassor amekimbilia Kituo cha Polisi Buguruni jijini Dar kutoa taarifa ya bintiye Saida Said (18) (pichani)kutoroshwa
nyumbani kwake siku chache kabla ya
ndoa.Alipofika kituoni hapo, mwanamke huyo alimtaja mtu mmoja kwa jina moja la Shaban kwamba ndiye aliyefanya kitendo hicho.

Mmoja wa ndugu ambaye hakupenda jina lake liandikwe alisema mama huyo amekuwa akihaha kwa binti yake kotoroshwa na mwanaume huyo
tangu Septemba 25, mwaka huu ambapo kila akimpigia simu hapatikana hewani.
Jeshi la polisi bado liko ndani ya msako mkali ili kuhakikisha binti huyo anapatikana na hatua za kisheria zinachukuliwa kwa mwanaume huyo.

Ndugu huyo alisema Saida alitarajiwa kufanyiwa kitchen part’ Oktoba 31, mwaka huu na kufuatia na ndoa Novemba 6 huku ikidaiwa kuwa, upande
wa bwana harusi michango inaendelea kama kawaida na walishalipa mahari yote.
Jalada la uchunguzi kuhusu kutoroshwa kwa bi harusi huyo linasomeka Kumbukumbu; BUR/
RB/10170/2014 KUTOROSHA.

Chapisha Maoni

 
Top