WINGA Gareth Bale ameweka rekodi mpya baada ya kushinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Wales kwa mara ya nne.
Wote Mark Hughes na John Hartson kila
mmoja alishinda tuzo hiyo Mwanasoka Bora wa Wales mara tatu, lakini hakuna aliyeshinda mara nne kabla.
Nyota huyo wa Real Madrid ametetea tuzo hiyo katika hafla ya chakula cha usiku ya tuzo za FAW iliyofanyika kwenye hoteli ya St David's mjini Cardiff- na saa ameba tuzo hiyo mara nne katika miaka mitano iliyopita.
Chapisha Maoni