0
Baraza la Maadili limetoa amri ya kukamatwa mara moja Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe.
Mrisho Gambo kwa kukaidi wito wa kufika mbele ya Baraza hilo kujibu tuhuma zinazomkabili.
Akizungumza baada ya kuahirisha kikao cha Baraza hilo lililoanza vikao vyake tarehe 9/10/2014, Mwenyekiti wa Baraza la Maadili Mhe Balozi Jaji (Mst.) Hamisi Msumi alisema kuwa amri hiyo imetolewa kwa mujibu wa fungu la 24
(4) la Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na.

13 ya 1995 ambayo imempa mamlaka Mwenyekiti wa Baraza hilo kutoa amri ya kukamatwa Kiongozi yeyote atakaekaidi wito wa kufika mbele ya Baraza
na kwa mujibu wa fungu hilo amri hiyo
itatekelezwa na Afisa wa Polisi.
Kiongozi huyo ambaye anatuhumiwa kwa makosa ya matumizi mabaya ya Madaraka aliitwa mbele
ya Baraza hilo ili aweze kujibu tuhuma
zinazomkabili.

Baraza la Maadili limeanza vikao vyake ambapo mashauri 19 ya viongozi wa kada mbalimbali wanaotuhumiwa kikiuka Sheria ya Maadili ya
Viongozi wa Umma kwa kutumia vibaya madaraka yao na kushindwa kuwasilisha Tamko la Mali na
Madeni yatasikilizwa.

Vikao hivyo vya Baraza la Maadili vinafuatia kukamilika kwa uchunguzi wa awali uliofanywa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma
kuhusu tuhuma za ukiukwaji wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma dhidi ya Viongozi husika.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Baraza hilo litaendelea na vikao vyake mpaka tarehe
17/10/2014.
Mwenyekiti wa Baraza la Maadili Mhe. Balozi Jaji (Mst.) Hamisi Msumi katikati akiwa na Wajumbe wa Baraza hilo Bibi Selina Wambura kushoto na
Bibi Hilda Gondwe kulia kabla ya kuanza kusikiliza Mashauri ya ukiukwaji wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma yaliyowasilishwa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.






Mwanasheria wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bw. Hassan Mayunga akifafanua jambo mbele ya Mwenyekiti wa Baraza la Maadili Mhe. Jaji Hamis Msumi.

Chapisha Maoni

 
Top