0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania amewapongeza wajumbe wa bunge maalum la katiba kwa kupendekeza katiba ambayo imejali
maslahi ya makundi yote wakiwemo wanawake na walemavu.

Rais Kikwete amesema hayo mjini Dodoma wakati alipokuwa akikabidhiwa katiba iliyopendekezwa na wajumbe wa bunge maalum la katiba mara baada ya kumalizika kwa vikao vya
bunge hilo maalum la katiba.
Kwa upande wake Rais wa Zanzibar Dkt.Ali Mohamedi Shein amesifu namna Zanzibar ilivyoshirikishwa ipasavyo katika kila hatua ya mchakato huo na kusema kwamba sasa wana
jukumu la kuweka utaratibu maalum ili waweze kuipigia kura katiba hiyo inayopendekezwa.

Kwa upande wake aliekuwa Mwenyekiti wa Maandishi, Andrew Chenge alisema katiba hiyo imejali maslahi ya wote na imetokana na rasimu ya pili ya katiba iliyowasilshwa katika bunge
maalumu la katiba ili kujadiliwa na kuiboresha.

Chapisha Maoni

 
Top