KIKOSI cha wachezaji 18 na viongozi 11 wa timu ya Taifa ya Benin, kimetua jijini Dar es Salaam tayari kwa mechi ya Kalenda ya FIFA dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumapili (Oktoba 12 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
Wachezaji wa timu ya Benin ambayo imefikia hoteli ya JB Belmont waliwasili jana (Oktoba 9 mwaka huu) Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa nyakati tofauti.
Kikosi hicho kitafanya mazoezi yake ya
kwanza leo (Oktoba 10 mwaka huu) saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Gymkhana. Benin watafanya mazoezi yao ya mwisho kesho (Oktoba 11 mwaka huu) saa 10 jioni Uwanja wa Taifa.Wachezaji walioko kwenye kikosi cha Benin ni.Stephane Sessegnon (West Bromwich Albion, Uingereza), Didier Sossa (USS Krake, Benin), Abdel Fadel Suanon (Etoile Sportive du Sahel,
Tunisia), Jodel Dossou (Red Bull Salzburg,
Austria), Sessi D’almeida (FC Girondis
Bordeaux, Ufaransa), Mohamed Aoudou (JS Saoura, Algeria) na Saturnin Allagbe (Niort, Ufaransa).
Steve Mounie (Montpellier, Ufaransa), Farnolle Fabien (Clermont Foot Auvergne 63, Ufaransa), Jordan Adeoti (Caen, Ufaransa), Michael Pote (Omonia Nikosia, Cyprus), David
Djigla (FC Girondis Bordeaux, Ufaransa) na Seidou Baraze (Kawkab Marrakech, Morocco).
Jean Ogouchi, Centre Mberie Sportif Club, Gabon), Nafiou Badarou (ASO Chlef, Algeria), Eric Tossavi (Avrankou Omnisport, Benin), Fortune Ore (USS Krake, Benin) na Seibou Mama (Aspac, Benin).
Nayo Taifa Stars inayodhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager leo (Oktoba 10 mwaka huu) itafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam saa 10 jioni.
Wakati huo huo, makocha wa Taifa Stars, Mart Nooij na wa Benin Didier Nicolle Olle watakuwa na mkutano na waandishi wa habari kesho (Oktoba 11 mwaka huu).
Mkutano huo utafanyika saa 5 asubuhi
kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika Jengo la PPF Tower.
Chapisha Maoni