CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) Mbeya mjini kimepongeza bunge maalumu kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kuchakata maoni ya wananchi na hatimaye kupatikana Katiba inayopendekezwa.
Kupitia kwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa wa CCM kutoka Mbeya Mjini (MNEC), Charles Mwakipesile chama hicho kilitoa pongezi za dhati
jana katika kikao maalumu na waandishi wa habari.
Mwakipesile alisema kupatikana kwa Katiba Inayopendekezwa, kunadhihirisha ahadi ya rais Jakaya Kikwete kuwapa Watanzania katiba mpya inakaribia kutimizwa sasa.
Alisema upatikanaji wa katiba hiyo
inayopendekezwa, ni sehemu ya picha ya kubeza wachache walioamua kukimbia bunge hilo na
kurudi mtaani kudai hakuna kitu cha msingi kilichokuwa kikifanyika mjini Dodoma.
“Mimi wale nawaita walioshuka kwenye basiblililokuwa linatupeleka kupata katiba mpya. Sasa kwa kuwa waliamua kushuka kwenye basi na kukimbilia kwa wananchi ili wawadanganye kwa
lengo la kuchochea vurugu ili tumwage damu, ni wakati kwao kurudi tena kwa wananchi waombebradhi”.
Aliendelea kusema, “Watanzania hawadanganyiki, sasa katiba inapatikana. Mwakipesile alisihi wananchi kutoa ushirikiano kwa kuikubali katiba inayopendekezwa mara itakapopelekwa kwao waipigie kura na kuwezesha kupatikana kwa
katiba mpya.
Aliunga mkono matamanio ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisema ni vema katiba ikapatikana kabla ya kupatikana kwa rais mpya.
Alisema hiyo itakuwa historia nzuri na yenye heshima kwa Rais Kikwete.
Alisema kukamilika kwa katiba kabla ya
kupatikana kwa rais mpya kutamwezesha rais ajae
kuanza kazi akitumia katiba hiyo na hakutakuwa na mzigo wa kuendeleza mchakato ulioanzishwa na kiongozi aliyemtangulia.
Chapisha Maoni