0
LIVERPOOL imepata ahueni na bila shaka kocha Brenden Rodgers atapumua leo. Hiyo inafuatia ushindi wa mabao 2-1 West Bromwich Albion Uwanja wa Anfield jioni hii.
Shukrani kwao, wafungaji wa mabao hayo, Adam Lalana dakika ya 45 na Jordan Henderson dakika ya 61, wakati bao pekee la WBA lilifungwa na Saido Berahino kwa penalti dakika ya 56.

Katika mechi nyingine za Ligi Kuu ya England jioni ya leo, Hull City imeifunga 2-0 Crystal Palace, mabao ya Mohamed Diame dakika ya 61 na Nikica Jelavic dakika ya 89.
Leicester City imetoka 2-2 na Burnley. Mabao ya Leicester yamefungwa na Jeffrey Schlupp dakika ya 34 na Riyad Mahrez dakika ya 41, wakati ya Burnley yamefungwa na Michael
Kightly dakika ya 39 na Ross Walace dakika ya 90.Swansea City imetoka sare ya 2-2 na
Newcastle United, mabao yake yakifungwa na Wilfried Bonny dakika ya 17 na Routledge dakika ya 50, huku ya wapinzani wao yakifungwa na Papiss Cisse dakika ya 43 na
75. Sundeland imeichapa 3-1 Stoke City, mabao yake yakitiwa kimiani na Cannor Wickham dakika ya nne, Steven Fletcher dakika ya 23 na 79, wakati bao la kufutia machozi la wapinzani wao limefungwa na Charlie Adam dakika ya 15.

Chapisha Maoni

 
Top