MSHAMBULIAJI Diego Costa ataukosa
mchezo wa Jumanne wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, timu yake Chelsea ikimenyana na NK Maribor Uwanja wa Stamford Bridge, amesema kocha Jose Mourinho.
Costa alikuwa nje ya kikosi cha Chelsea jana kikishinda 2-1 dhidi ya Crystal Palace katika Ligi Kuu ya England na ataendelea kupata tiba kwa muda.
Mpachika mabao huyo wa zamani wa Atletico Madrid aliumia akiichezea timu yake ya taifa Hispania na Mourinho amesikitishwa mno na kumkosa nyota wake huyo mkali wa mabao."Baada ya mechi na Arsenal akaenda timu ya taifa, akacheza mechi mbili kubwa na amerudi akiwa na hali ambayo hawezi kucheza,"amesema Mourinho.
"Nafikiri atakuwa katika hali nzuri katikati ya Novemba kurejea katika timu ya taifa.
Tutakuwa makini mno juu yake. Atacheza kwangu atakapokuwa huru baada ya kumaliza majukumu ya timu ya taifa,"amesema.
Chapisha Maoni