LIVERPOOL imeshinda 3-2 dhidi ya Queens Park Rangers jioni ya leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa ugenini.
Mabao ya Liverpool yamefungwa na Richard Dunne aliyejifunga dakika ya 67, Philip Coutinho dakika ya 90 na Steven Caulker aliyejifunga pia dakika hiyo hiyo ya 90.
Richard Dunne leo ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kujifunga mabao 10 katika historia ya Ligi Kuu ya England.
Raheem Sterling alianza leo kwenye kikosi cha Liverpool na kocha wa England, Roy Hodgson akamshuhudia kutokea jukwaani. Mario Balotelli alikosa bao akiwa amebaki yeye na nyavu, baada ya kupiga juu akiwa
umbali wa mita tatu wakati huo matokeo bado yapo sare.
Chapisha Maoni