0
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Chelsea,
Demba Ba usiku huu amefunga kwa penalti kuipatia timu yake Beskitas sare ya 1-1 ugenini na Tottenham Hotspur Uwanja wa White Hart Lane katika mchezo wa Kundi C Europa League.

Demba alifunga penalti hiyo dakika ya 89, akimtungua kipa hodari Hugo Lloris baada ya Vlad Chiriches kuunawa mpira kwenye boksi. Tottenham ilipata bao lake mapema dakika ya 27 kupitia kwa Harry Kane na Lloris alijitahidi
kuulinda ushindi huo kwa kuokoa
michomo mingi ya hatari, kabla ya Chiriches kuwazawadia penalti wapinzani.

Chapisha Maoni

 
Top