Kama wiki mbili zimepita toka jeshi letu pendwa litupige mkwara juu ya matumizi ya sare zake au zinazofanana na hizo kwa mtu ambae si askari..
Kwamba ukivaa tu basi umevunja sheria na inapaswa uadhibiwe mara moja, either mahakamani au ‘wapigwe tu’.. Hilo linapewa nguvu na taarifa ya juzi kati jamaa kulazimishwa kuoga maji ya barabarani maeneo ya kariakoo
baada ya mjeda mmoja kumnyaka na nguo zinazofanana na zao..
Sasa cha ajabu mbona juzi katika tamasha la Fiesta mwanamziki Diamond na timu yake pamoja na Ney anayewatega, wameonekana wazi wakiwa na sare hizo tena wamezivaa hovyo hovyo kata K wakinengua jukwaani.??? Au hiyo sheria
inamgusa nani? Huyu kijana akiwa na ufahamu kuwa television ya
taifa inaonyesha hili tamasha lao kavaa SARE ZA JESHI tena full kuanzia viatu mpaka kofia.
Wasanii ni Mfano wa Kuiga, Sasa hawa
wanafundisha nini watu wengine?
Hii ni Dharau
Chapisha Maoni