0
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed
Shein


Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed
Shein, amepata mpinzani iwapo ataamua tena kugombea nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu ujao mwakani, baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Tadea, Juma Ali Khatib (50), kutangaza nia ya kuwania nafasi hiyo visiwani humu.
Mgombea huyo ni watatu kujitokeza
hadharani na kutangaza nia ya kuwania
nafasi hiyo, baada ya katibu mkuu wa
CUF, ambaye ni Makamu wa Kwanza wa
Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, kutangaza nia hiyo akifuatiwa na Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed aliyetangaza pia nia hiyo.

Hamad Rashid alitangaza nia na kusema
kuwa atawania nafasi hiyo kupitia CUF,
mgombea binafsi au kwa tiketi Chama
cha Alliance for Democratic Change
(ADC).
Ikiwa Maalim Seif atawania tena nafasi
hiyo, itakuwa ni mara ya tano tangu
mwaka 1995, ulipoanza mfumo wa
vyama vingi mwaka 1992.


Uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama
vingi ulifanyika mwaka 1995, ambapo
Seif alishindwa kwa mara ya kwanza na
Dk Salmin Amour Juma wa CCM huku
mara mbili akichuana na Dk Amani
Karume na kushindwa pia.
Katika maelezo yake kuhusu hatua hiyo,
Khatib alisema amechukua uamuzi huo
kutokana na matatizo yanayowakabili
wananchi wa Zanzibar.
“Matatizo ya Wazanzibar ndiyo
yaliyonisukuma kuchukua fomu ya urais
wa Zanzibar. Huduma za jamii
zimezorota, kuongezeka kundi la vijana
wasio na ajira mitaani, wazee kuishi
mazingira magumu na ongezeko la
ombaomba visiwani Zanzibar,”alisema.

Alisema pamoja na Serikali ya Umoja wa
Kitaifa (SUK), kuundwa Zanzibar miaka
minne iliyopita, utendaji wa Serikali
katika kuutumikia umma hauonekani.
“Rais anahitaji kuangalia upya viongozi
na watendaji aliowateua na kuwapa
majukumu. Nafikiri wameshindwa
kubuni mipango ya kuwatumikia watu.
Utendaji wa watu wanaomsaidia
haujengi taswira halisi, baadhi yao
wameshindwa kusimamia majukumu yao ipasavyo,” alisema Khatib.

Alisema pamoja na kuwepo sheria nzuri,
kumekosekana utashi na usimamizi
makini, juhudi na dhamira ya wazi na
kutokuwepo utendaji unaotarajiwa.

Chapisha Maoni

 
Top