0
Shirikisho la kandanda Ulimwenguni ( FIFA ) hii leo limetangaza jumla ya majina 23 wa wachezaji wa soka watakaowania tuzo ya Mchezaji bora wa
FIFA " Ballon d'Or " kwa mwaka 2014.
Hata hivyo kabla ya mwezi wa 12, majina hayo yatachujwa na kubakizwa majina ya wachezaji 3 ambao ndio wataingia katika kinyang'anyiro cha
kuwania tuzo hiyo.

Mshindi atakabidhiwa tuzo hiyo January 12' 2015 mjini Zurich, Uswis.Majina hayo ya wachezaji na nchi wanazotoka ni kama ifuatavyo:-
Gareth Bale (Wales), Karim Benzema
( Ufaransa ), Diego Costa ( Hispania ), Thibaut Courtois ( Ubelgiji ), Cristiano Ronaldo ( Ureno ), Angel Di Maria (Argentina ), Mario Goetze ( Ujerumani )

Wengine ni Eden Hazard ( Ubelgiji ), Zlatan Ibrahimovic (Sweden), Andres Iniesta ( Hispania ), Toni Kroos ( Ujerumani ), Philipp Lahm ( Ujerumani ), Javier Mascherano (Argentina ), Lionel Messi (Argentina ).

Pia wamo Thomas Mueller ( Ujerumani ), Manuel Neuer ( Ujerumani ), Neymar ( Brazil ), Paul Pogba ( Ufaransa ), Sergio Ramos ( Hisapnia ), Arjen Robben ( Uholanzi ), James Rodriguez
(Colombia), Bastian Schweinsteiger
( Ujerumani ), na Yaya Toure (Ivory Coast).

Chapisha Maoni

 
Top