Mtangazaji mahiri Gardner.G. Habash,amejiunga na kituo cha Radio kinachokuja kwa kasi hivi sasa
EFM 93.7 cha jijini Dsm ili kuongeza nguvu katika kikosi chao.
Akizungumza leo na waandishi wa habari afisa habari wa EFM Kanky Mwaigomole amesema
wameamua kumchukua Gardner kwasababu ni miongoni mwa watangazaji hodari nchini mwenye
kipaji cha hali ya juu hivyo kuongeza chachu ya mafanikio katika kituo hicho kipya.
“Gardner ataendesha kipindi kiitwacho Ubaoni kuanzia saa tisa alasiri mpaka saa moja kamili jioni kuanzia Jumatatu ya tarehe 03 mwezi wa 11 mwaka huu”alisema Kanky.
Gardner alimaarufu “KAPTENI” alianza kazi na kituo cha Radio Clouds fm na baadaye Times fm ambapo kwa sasa ametua Efm akitanguliwa na
wakongwe kama Dj Majey,Dizzo One,Sos B,Denis Ssebo,Maulidi Kitenge,Omari Katanga,Scholastica Mazula na Kanky Mwaigomole.
Asante,
Meneja Uhusiano. Kanky Mwaigomole.
Chapisha Maoni