0
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape
Nnauye akizungumza na waandishi wa
habari kwenye ukumbi wa
Sekretarieti,makao makuu ya Chama Ofisi Ndogo Lumumba jijini Dar es Salaam.

NA BASHIR NKOROMO
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimepokea kwa furaha Chama cha Frelimo kuibuka na ushindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika
Oktoba 15, mwaka huu. Katika uchaguzi huo, aliyekuwa mgombea kwa tiketi ya Frelimo, Mhe Filipe Nyusi ameibuka kidedea na sasa ndiye Rais Mteule wa Msumbiji ambaye baada ya
kuapishwa atashika mikoba itaakayoachwabna Rais anayemaliza muda wake, Armando
Gwebuza.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, katika ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (Pichani), amesema,
CCM imepokea ushindi huo kwa furaha
kubwa kutokana na undugu wa damu
uliopo baina yake na Frelimo kwa mikaka mingi.

"Chama Cha Mapinduzi kilifuatilia kwa
karibu kwa kuwa CCM na Chama cha
Frelimo ni vyama ndugu vyenye historia
moja na ya pamoja ya Ukombozi Kusini
mwa Afrika. Historia hiyo ndiyo
iliyomfanya Rais Mteule wa nchi hiyo
Ndugu Filipe Nyusi mara baada ya
kuteuliwa kwake na Frelimo kugombea
Urais, nchi ya kwanza kuitembelea kuwa
Tanzania", alisema Nape na kuongeza;
"Ikumbukwe kwamba huyu si mgeni hapa Tanzania. Kama wanaharakati wengine wa ukombozi, Ndugu Nyusi aliishi Tanzania, anaongea vizuri Kiswahili na anaichukulia
Tanzania ni nyumbani".

Alisema kwa mnasaba huo, Chama Cha
Mapinduzi na Watanzania kwa ujumla
wana kila sababu ya kushangilia ushindi
walioupata ndugu zao wa Frelimo, kwa
kuwa ushindi huo ni wa wote.
"Tunampongeza sana Rais Mteule Filipe
Nyusi kwa kupeperusha vema bendera ya Frelimo. Matokeo ya Uchaguzi
yamedhihirisha imani kubwa waliyonayo
wana-Msumbiji kwa Frelimo na kwa Rais Mteule Filipe Nyusi", alisema Nape.
Nape amesema CCM ina imani kwamba
chini ya uongozi imara wa Mwenyekiti wake
Dk. Jakaya Kikwete, na Rais Mteule Filipe Nyusi, uhusiano kati ya vyama vya CCM na Frelimo utaimarika na kustawi.
Kadhalika Chama Cha Mapinduzi
kimempongeza Armando Guebuza kwa
kuiongoza Frelimo na Taifa lake vema na
kukamilisha uongozi wake kwa mafanikio makubwa.

"Anapoanza kipindi hiki cha uongozi wa
Taifa lake, sisi wana-CCM tunamtakia
Ndugu Nyusi afya njema, busara, maarifa
na uongozi uliotukuka", alisema Nape.
Alisema, CCM itasimama pamoja na
Frelimo katika kuendeleza urithi ulioachwa na waasisi wa vyama vyao, Mwalimu Julius Nyerere na Samora Machel.

Chapisha Maoni

 
Top