Mwanamke nchini Ufaransa, juzi amefunga ndoa na mwanae wa kambo baada ya kusuguana na mamlaka za nchini humo kuhusu haki yake ya
kuolewa.
Elisabeth Lorentz, 48, amefunga ndoa na Eric Holder, kanisani kwenye kijiji kidogo Dabo huko Alsace-Lorraine, kaskazini mashariki mwa Ufaransa. Ms Lorentz alikutana na baba yake na Holder mwaka 1989, wakati huo akiwa na miaka
24.
Wawili hao walipata mtoto wa kike mwaka 1997 – ambaye ni dada yake na Holder lakini pia mtoto wake wa ubatizo.
Holder pia alikuwa na mtoto kipindi hicho. Ms Lorentz aliolewa na baba yake Holder mwaka 2003, lakini walitengena baada ya miaka mitatu.
Ms Lorentz ameviambia vyombo vya habari kuwa baada ya kuachana na mume wake, mwanae wa
kike ambaye alikuwa na miaka 9 aliumizwa vibaya na alikuwa akilia kila siku. “Hapo ndipo Eric akawa msaada mkubwa kwetu na uhusiano
ulizaliwa,” alisema.
Holder, ambaye anasema alijitahidi kumliwaza dada yake aliyekuwa pia mtoto wake wa kuzaliwa na sasa mwanae wa kambo, alisema: ‘Baada ya
baba kumwacha mama, nilihisi kutengwa. Nilijua alivyojisikia.
Haikuchukua muda Holder akaamua kumwomba uchumba mama yake wa kambo. Hata hivyo walikumbana na kikwazo kwakuwa sheria za Ufaransa zinakataza ndoa ya watoto na wazazi wa
kambo.
Chapisha Maoni