0
Maofisa wa polisi nchini Kenya wameeleza kwanini waliamua kumkamata muimbaji wa dancehall wa Kenya, Mohamed Swabir aka Redsan
weekend iliyopita.
Polisi wamesema msanii huyo pamoja na washkaji zake akiwemo producer wake, Sappy ambaye ni Mtanzania, waliwasili kwenye viwanja vya ‘Nairobi International Trade Fair’ siku ya
Ijumaa tayari kwa show lakini waligoma
kukaguliwa.

Hiyo ni baada ya mmoja wao kuonekana na bunduki na hivyo polisi kuhisi ni magaidi au majambazi.
“Tulitakiwa kulikagua kundi hilo kwaajili ya usalama wa watu waliokuwepo hapo. Walikataa kukaguliwa na kuondoka kitu ambacho kiliwapa wasiwasi polisi,” alisema OCPD wa Kilimani, Peter
Katam.

Redsan na wenzake walilala kituoni hapo kwa siku moja.

Chapisha Maoni

 
Top