Ligi Kuu England ukipambwa na bifu kubwa kati ya Mameneja wa Timu hizo.
Mwezi Februari, Meneja wa Chelsea Jose Mourinho alimwelezea Meneja wa Arsenal Arsene Wenger kama
Mtu ‘spesho wa kushindwa’ na hii Leo Mourinho alikataa kuomba radhi kwa matamshi hayo.
Msimamo huo umeleta chachu kubwa kwa ajili ya Mechi hiyo ya Jumapili huku Chelsea wakiwa kileleni mwa Ligi wakiwa wameshinda Mechi 5 na Sare moja na wako Pointi 6 mbele ya Arsenal ambao wako Nafasi ya 4 wakiwa wameshinda Mechi 2 na Sare 4.
Mourinho ameueleza msimamo wake: “Yale yalikuwa matokeo ya kitu. Haikuwa makusudi kusema kitu. Sikuombwa radhi. Sitaomba radhi.” Mourinho amesema huu ni wakati wa kusahau na
kusonga mbele.
Chapisha Maoni