MSHAMBULIAJI Lionel Messi amesema
kwamba anafikiria zaidi kushinda mataji na Barcelona kuliko kushindana na nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo kwa tuzo binafsi.
Wakali hao wawili wa La Liga, ambao
wamekuwa wakichuana kwenye tuzo ya
Mwanasoka Bora wa Dunia kwa miaka sita iliyopita, pia wanachuana kwa ufungaji wa mabao Hispania na Ulaya.
Pamoja na hayo, Messi amejiweka kando katika ushindani huo kwa kusema kwamba hapendi kushindana na nyota huyo wa Ureno."Kushindana na Cristiano? Sihisi kushindana naye au yeyote yule," amesema Messi. "SI juu ya tuzo binafsi. Nataka kuisaidia timu yangu. Sifikirii kuhusu nafasi yangu kwenye
historia ya soka. Nachotaka ni kuendelea kuwa vizuri na kushinda mataji na timu yangu," amesema.
Messi anaamini mchezaji mwenzake wa
Barcelona, Neymar ana nafasi nzuri ya
kuwapiku wote yeye na Ronaldo na kuwa mchezaji bora duniani.
"Ndiyo mwaka wake wa pili tu hapa, lakini nina uhusiano naye mzuri ndani na nje ya Uwanja. Ni kijana babu kubwa.
Kwa sababu ya ubora wake, nafikiri Neymar atakuwa bora duniani. Ni mchezaji babu kubwa ni furaha kucheza katika timu yangu,".
Chapisha Maoni