0
MWANASOKA Lionel Messi atapandoshwa tena kizimbani kwa kesi ya ukwepaji kodi baada ya Jaji kuitupilia mbali rufaa ya nyota huyo wa Barcelona nchini Hispania.

Mshindi huyo mara nne wa Ballon d'Or (tuzo ya mwanasoka bora wa dunia) na baba yake, Jorge Messi, wanatuhumiwa kukwepa kiasi cha Pauni Milioni 3.4 cha kodi kati ya mwaka 2007 na 2009.

Muargentina huyo anarudi katika wakati
mgumu tena kwa ajili ya kesi hiyo, ambayo awali ilionekana kama angeshinda kwa urahisi- lakini Jaji wa Hispania amesema taarifa yake jana kwamba mambo ni
magumu.

Chapisha Maoni

 
Top