Kuanzia Ijumaa iliyopita kulikuwa na taarifa kuwa mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam imemzuia Davido kutumbuiza kwenye show ya
Fiesta jijini Dar es Salaam kwakuwa msanii huyo alikuwa ameshaingia mkataba wa show nyingine
na kituo cha redio cha Times FM kilichokuwa kimepanga kuwa na tamasha November 1.
Hata hivyo huenda Clouds FM walimpa ofa kubwa zaidi msanii huyo kiasi cha kuamua kuuvunja mkataba wake na Times FM. Kufuatia suala hilo, makampuni hayo yalipelekana hadi mahakamani kiasi cha mahakama kutoa amri ya kuwa Davido asipande.
Kwakuwa Davido hata hivyo
alitumbuiza, huenda makampuni hayo yalikaa chini na kupata suluhu.
Davido ametumia Instagram kutoa shukrani zake baada ya kuwa sehemu ya wasanii waliotumbuiza Jumamosi iliyopita.
“Kwaheri TANZANIA 26464 ! It was great sharing the stage with @troubleman31 … Thank you clouds Fm for making it possible! And bless my brother @diamondplatnumz for welcoming me
well.”
Chapisha Maoni