Meneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale amesema haoni kama wameathirika na kundi la watu waliomzomea msanii huyo wakati
akitumbuiza Jumamosi hii kwenye show ya Serengeti Fiesta, Leaders Club jijini Dar es Salaam.
Tale amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM kuwa walikuwa na taarifa kuhusu mpango huo hata kabla ya show na hivyo walijiandaa.
“Tulikuwa tumemjenga kisaikolojia, kwahiyo hiyo ni sehemu ya kazi na mashabiki ingekuwa wanapiga kelele kama tumekosea show kweli,
lakini sio hivyo. Show ilikuwa sawa,” amesema Tale.
“Tunachojua sisi msanii wetu anafanya vizuri na. sasa hivi nguvu zetu tumeelekeza katika tuzo.
Wananchi wakaze kumpigia kula katika tuzo Channel O na MTV, sie sasa hivi tunasonga mbele, tunachojua chema chajiuza, kibaya chajitembeza.”
Chapisha Maoni