Wanawake MUNGU awasaidie sana Mjue kujenga Mahusiano binafsi ya karibu na MUNGU mwenyewe kuliko kutegemea sana kuombewa hovyo hovyo,Kisa tu
Umeambiwa na Rafiki yako kwamba
yuko Apostle flani ana Upako sana.
Ndio ni kweli mna Matatizo mengi
yamewasonga yakiwemo Ndoa zenu
Watoto wenu,Biashara zenu,na
Kadharika,Na mara nyingi nia yenu ni
kufunguliwa kwenye hivyo vifungo
vinavyowasumbua.
Na shetani yuko karibu sana nanyi kwasababu anajua Nguvu iliyomo ndani yenu, ila wengi wenu hamjielewi.Ndio maana Mnafanyiwa vitu vingi sana kwa jina la kukombolewa na baadhi ya Watumishi kwa imani kwamba Mtapona.Na ndio maana kila huduma maombezi Mmejaa
nyie na Ndio maana inakuwa rahisi sana
kwenu kudhurumiwa mambo mengi kwa
kujenga imani kubwa sana kwa watu
kuliko BABA yenu.
Hebu tazama picha kama hii,Mumeo
akikukuta unafanyiwa Maombi ya Staili
hii "Atakuelewa kweli!?
Jifunzeni kumlilia MUNGU vyumbani
mwenu na Mkumbusheni ahadi zake juu
ya Maisha yenu na vizazi vyenu.
Chapisha Maoni