Kweli waliosema mwisho wa ubaya ni aibu waliona mbali sana hivyo ndiyo kituo cha Clouds Fm Radio & Prime Prodution walivyoanza kujishushia hadhi walijijengea miaka mingi nchini
baada ya kumrubuni msanii toka Nigeria Davido kuja kufanya shoo kwenye onesho la Fiesta wakati tayari alishaanza kusikika kwenye kituo cha radio Times Fm 100.5 kwa jingo kama atakuwepo Tanzania Nove 1. 2014.
Katika sakata hilo mashabiki wa kituo hicho cha Clouds Fm wameongea mengi na kutoa ushauri kwa viongozi wa kituo hicho, ambapo Jackline Mushi mkazi wa Ukonga Jijini Dar alikuwa na haya ya kusema " Kiukweli Clouds kwa hili
wamejidhalilisha walishindwa kuandaa msanii wao hadi wamdandie msanii ambae tayari ameshaingia mkataba na kituo kingine hadi Mahakama
inaiingilia kati hii ni aibu kwa kampuni kama hiyo yenye uwezo mkubwa sana"
Alisema msichana huyo
Aidha nae Edwini Chiwanga ambae ni Polisi Kilwa Road alikuwa alisema" Kweli mwisho wa ubaya ni aibu Clouds iliheshimika sana miaka mingi lakini
kwa uletaji wasanii lakini naona sasa imeshaanza kupoteza sifa Mungu amewaumbua" Alisema Maoni yalikuwa mengi sana lakini hata hivyo na
wako ambao waliomba hifadhi ya majina yao walisema kuwa kituo hicho cha Clouds sasaBkinatakiwa kukubali chalenji kwenye uandaji matamasha Times ni kampuni ya kitanzania tena
na Clouds pia hivyo ni vyema kushirikiana kwenye
masuala hayo ya burudani ili kuleta sifa njema kwa nchi yetu kuliko kutaka kukomoana na mwisho ni aibu kama hizi Mahakama sasa imetoa amri hiyo na sijui itakuaje.
Chapisha Maoni