0
Mratibu wa shughuli za Umoja wa mataifa kuhusu ugonjwa wa ebola Davis Nabarro ametetea juhudi za kimataifa za kupambana na ugonjwa huo
magharibi mwa afrika.

Bwana Nabbaro alikuwa akijibu shutma kutoka kwa shirika la madaktari wasio na mipaka MSF lililosema kuwa ahadi za misaada hazijakuwa na mafaniko yoyote katika vita dhidi ya ugonjwa wa
ebola.
Ameiambia BBC kuwa mipango iko njiani ya kutoa vitanda 4000 kwa wagonjwa wa ebola ifikiapo mwezi ujao. Matamshi yake yanajiri baada ya ripoti ya ndani ya shirika la afya duniani inayosema kuwa WHO imeshindwa kuzuia kusambaa kwa ugonjwa wa
ebola.

Chapisha Maoni

 
Top