0
KLABU ya Manchester City imevuliwa
ubingwa wa Kombe Ligi, kufuatia kuchapwa mabao 2-0 na Newcastle Uwanja wa Etihad ambayo sasa inakwenda Robo Fainali.

Rolando Aarons alifunga bao la kwanza
akimtungua kipa wa tatu, Willy Caballero
dakika ya sita kabla ya Moussa Sissoko
kufunga la pili dakika ya 75.
Manchester City sasa inatimiza mechi tatu bila kushinda na mchezo ujao itamenyana na mahasimu wa Jiji, Man United Jumapili.

Kikosi cha Man City kilikuwa; Caballero,
Sagna, Demichelis, Mangala, Kolarov,
Fernandinho, Toure/Navas dk59, Milner,
Jovetic, Silva/Nasri dk8/Aguero dk69 na
Dzeko.

Newcastle; Elliot, Janmaat/Sissoko dk64, Coloccini, Dummett, Haidara, Abeid, Obertan, Taylor, Colback, Aarons/Ameobi dk45 na Armstrong/Riviere dk64.

Chapisha Maoni

 
Top