BAO la dakika ya 87 la kiungo Daley Blind limeinusuru Manchester United kulala mbele ya West Brom Albion baada ya kupata sare ya 2-2 ugenini katika mchezo wa Ligi Kuu England usiku huu.
Blind alifunga bao zuri kutoka umbali wa mita 23, likiwa bao lake la kwanza tangu ajiunge na Mashetani hao Wekundu msimu huu.
Stephane Sessegnon aliyeshindwa kufurukuta mbele ya Tanzania, Taifa Stars akiichezea Benin ikifungwa 4-1 katika mchezo wa kirafiki Oktoba 12 Uwanja wa Taifa mjini Dar es
Salaam, leo aliifungia WBA bao la kwanza dakika ya nane akimalizia krosi ya Andre Wisdom.Marouane Fellaini aliyetokea benchi dakika ya 46 kuchukua nafasi ya Ander Herrera, aliisawazishia Manchester United dakika ya 48 akimalizia pasi ya Angel di Maria.
Mzaliwa wa Burundi, Saido Berahino
akaifungia bao lililoelekea kuwa la ushindia West Brom dakika ya 66 akimalizia pasi ya Chris Brunt, kabla ya Blind ‘kuchomoa’ dakika za lala salama.
Kikosi cha Manchester United kilikuwa: De Gea, Rafael, Jones, Rojo, Shaw, Blind,
Herrera/Fellaini dk46, Januzaj, Mata/Falcao dk72, Di Maria/Ashley Young dk76, Van Persie
West Brom: Myhill, Wisdom, Lescott, Dawson, Pocognoli, Gardner, Brunt, Morrison, Dorrans, Sessegnon/Youssuf Mulumbu dk86 na Berahino.
Chapisha Maoni