0
Jumatatu ya wiki hii Jeshi la Wananchi Tanzania, JWTZ, lilitoa tamko kuhusu wananchi kumiliki au kuvaa sare za jeshi hilo.

Japo tamko hilo la JWTZ limetoka kwa ufupi bila kuweka wazi kwanini wameamua kulitoa tena wiki
hii, ni wazi kuwa limetokana na wasanii kadhaa wakiwemo Diamond na dancers wake, Chege na Nay wa Mitego kuvaa sare hizo kwenye show ya Serengeti Fiesta iliyofanyika kwenye viwanja vya
Leaders Club jijini Dar es Salaam.
Tunahisi katika taarifa hiyo, JWTZ walitakiwa kuweka wazi kuhusu nguo zao kutumika kwenye show hiyo.

Kuna tetesi kuwa wasanii hao walipewa kibali maalum kutoka jeshi hilo kufanya hivyo. Kama walimpa kibali Diamond na wasanii wengine, tunadhani lilikuwa ni jambo jema kama jeshi hilo lingeweka wazi kuwa walitoa kibali kwa wasanii
hao kutumia sare zao.

Ama kwenye taarifa hiyo fupi kwa vyombo vya habari walipaswa kusema kuwa ‘mwananchi anaweza kutumia sare hizo katika matumizi yake
iwapo atakuwa na kibali maalum kutoka JWTZ’ . Iweje leo umwambie mwananchi kuwa asimiliki wala kuvaa sare hizo wakati jana tu aliwashahudia wasanii wakiwa wamezivaa jukwaani?
Na mbona kama jeshi linakatakaza, kwanini hatujasikia hatua yoyote imechukuliwa kwa wasanii hao? Mbona kwenye taarifa kwa vyombo vya habari, jeshi halijasema kuwa Diamond na
wasanii wengine wamefanya kosa? Au akifanya msanii anayejulikana hilo sio kosa?
Kama walipata kibali kwanini JWTZ halijasema hivyo ili tufahamu kuwa nguo hizo zinaweza kuvaliwa pale tu kibali maalum kitakapotolewa! Taarifa hiyo iliyotoka haijaweza kujibu maswali
muhimu waliyonayo wananchi wengi kuhusiana na uhalali wa kuvaa sare za kijeshi.

Chapisha Maoni

 
Top