Oscar Pistorius amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kwa kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp, baada ya timu yake ya utetezi
kushindwa kumshawishi jaji Thokozile Masipa kumpa kifungo cha nje.
Pia alihukumiwa miaka mitatu, iliyojumuishwa kwenye hukumu ya miaka mitano baada ya kushoot pistol kwenye mgahawa huko Johannesburg, January 2013. Hukumu hiyo
inaanza mara moja.
Mwezi uliopita, Pistorius alipatikana na hatia ya kuua bila kukusudia na kusababisha kifo cha mpenzi wake Reeva Steenkamp pamoja na
kupatikana na hatia ya kutumia silaha kizembe katika tukio tofauti.
Judge Masipa alisema kwenye hukumu hiyo kuwa alitumia majaji wengine wawili kumsaidia lakini uamuzi wa hukumu hiyo ulikuwa wake
mwenyewe.
Chapisha Maoni