0
Msanii wa kundi la Wanaume Family YP aliyefariki usiku wa kuamkia leo kwa ugonjwa wa kifua, anatarajiwa kuagwa kesho (October 22) kwenye viwanja vya TCC Chang’ombe na baada ya hapo
atazikwa katika makaburi ya Chang’ombe karibu na maduka mawili.

Akizungumza na mtandao huu jioni hii, kiongozi wa kundi la TMK Wanaume Family amesema mpaka sasa wapo kwenye maandalizi ya mazishi
yatakayofanyika kesho saa kumi jioni.
“Kwajinsi ratiba ilivyo msiba utakuwa nyumbani kwa baba yake, kwenye nyumba ya marehemu baba yake kwahiyo kesho tunatarajia tukiweza
tumuage pale Chang’ombe na baada ya hapo tutazika kwenye makaburi ya Chang’ombe hapo karibu na maduka mawili,” amesema Fella.

Chapisha Maoni

 
Top