Miss Sinza aliyeshiriki Miss Tanzania 2011, Husna Maulid amekanyaga skendo ya wizi baada ya kudaiwa kuwahi ‘kumdokolea’ aliyekuwa mpenzi
wake, Mwani Rajabu ‘Mkongo’.Chanzo
kilichoomba hifadhi ya jina lake kilidai kuwa, kutokana na tabia hiyo Husna alitoswa na mpenzi wake huyo ambaye ni raia wa Kongo.Baada ya
kuzinyaka habari hizo mapaparazi wetu
walimtafuta Mwani ambaye yupo Bongo kwa sasa na alipopatikana alisema:
“Yaani Husna hana kasoro nyingine zaidi ya hiyo kwani amekuwa akinifanyia hivyo tunapokuwa hotelini, sasa tabia yake ilinichosha nikaamua
kuachana naye.”
Kwa upande wake Husna alipoulizwa kuhusiana na tuhuma hizo alikanusha vikali na kusema hajawahi kuwa mwizi bali anazushiwa.
“Mimi siyo mwizi na sijawahi, naomba muulize vizuri huyo Mkongo kama nilishawahi kumuibia nini,” alisema Husna.
Chapisha Maoni