waliotaka kufanya mkutano wa ndani.
Mkutano huo ulikuwa uhutubiwe jana na
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Halima Mdee ambaye yuko ziarani katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Msafara wa Mdee uliwasili katika Kijiji cha Karukwara, Kata ya Isingiro saa 8:35 mchana na kwenda kusaini kitabu cha wageni katika ofisi za chama hicho na viongozi wenzake, huku nje
wakisubiriwa na wafuasi wao.
Mdee alipomaliza kusaini alitoka nje na naibu katibu mkuu wa Bawacha Kyerwa, Kunti Yusuph ambaye aliwaeleza wafuasi hao kuwa Mdee hataweza kuhutubia kwa kuwa polisi wamezuia
kufanyika mkutano.
Ilipofika saa 8:55 mchana polisi walifika eneo hilo na kuwataka wafuasi hao kutawanyika lakini hawakukubali, hivyo iliwalazimu polisi kuwatawanya wafuasi hao kwa kutumia mabomu
ya machozi jambo lililowafanya wafuasi kuanza kuwarushia mawe askari hao. Awali, mwenyekiti wa Chadema Kyerwa, Deus Rutakyamirwa alisema polisi walizuia kufanyika mkutano wa aina yoyote usiku wa kuamkia jana.
“Tulipeleka barua ya taarifa ya kufanyika kwa mkutano wa ndani Oktoba 25 mwaka huu, lakini juzi saa 7 usiku, OCD alinipigia simu akinitaka niende kituoni kuna barua yangu, mimi nilijibu
siwezi kwenda kwa kuwa nilikuwa nimelala.
“Alinieleza kuwa anakuja kwangu kuniletea barua hiyo, alikuja hadi kwangu na kunipa barua ya
kuzuia mkutano wetu, lakini nilimuuliza kwa nini wanazuia mkutano usiku wakati msafara upo njiani? Hakunijibu,”alisema Rutakyamirwa.
Chapisha Maoni