0
Mamia ya watu kwa shangwe na vigelegele
wamemkaribisha Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta baada ya kurejea kutoka kikao chake katika mahakama ya kimataifa ya ICC mjini the Hague.
Kenyatta alihudhuria kikao maalum katika mahakama hiyo Jumatano, na kuwa Rais wa kwanza aliye mamlakani kufika katika mahakama
hiyo.
Mahakama hiyo ilimtaka afike mbele yake kutokana na malalalmsihi kutoak kwa kiongozi w amashitkaka kuwa serikali ya Kenya inaficha
ushahihidi kuhusiana na kesi inayomkabili. Alikanusha madai ya uhalifu dhidi ya binadamu
wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi nchini Kenya mwaka 2007 ambayo yalisababisha vifo vya
watu 1,200 na kuwaacha wengine zaidi ya laki sita bila makao.

Kenyatta alipokelewa na idadi kubwa ya watu waliokuwa wanacheza densi pamoja na gwaridde
la heshima. Asubuhi na mapema, wafuasi wake walipanga
foleni kwenye barabara ya kutoka uwanja wa kimataifa wa ndege mjini Nairobi.
Walipeperusha bendera na kusikika wakiimbia kwa shangwe na kumsifgu Kenyatta wakisema kuwa
Rais wao hana hatia. Rais aliwahutubia kwa mda mfupi umati huo wa
watu ambao waliombwa kufika kumpokea rais na waziri wa usalama.

Mwandishi wa BBC aliyefika kushuhudia Rais huyo akiwasili nchini alisema kuwa Kenyatta ana wafasui
wengi.

Chapisha Maoni

 
Top