0
Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania,.Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Biswalo Mganga kuwa Mkurugenzi wa
Mashitaka (DPP) nchini.

Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar Es Salaam, jana, Jumatatu, Oktoba 6, 2014, na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Bwana Peter Ilomo inasema kuwa
uteuzi huo umeanza Ijumaa iliyopita, Oktoba 3, mwaka huu, 2014.

Kabla ya uteuzi wake, Bwana Mganga alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka na Wakili wa Serikali Mfawidhi.

Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
6 Oktoba, 2014

Chapisha Maoni

 
Top