Akizungumza na gazeti la Mtanzania Wakazi alikiri kwamba yeye ndiye meneja mpya wa Jaydee japo hakuwa tayari kueleza lolote kuhusu ndoa ya
binamu yake Jaydee na Gardner kwa maelezo kwamba yeye si msemaji wao katika masuala ya mapenzi na ndoa yao.
“Mimi sijui chochote, maana nilipokwenda Marekani niliwaacha wakiwa wachumba, lakini nilipokuwa huko nikasikia wameoana, niliporudi
nikawakuta tayari wapo katika ndoa na nimeanza kazi ya umeneja wa Jaydee si muda mrefu, hivyo sijui mahusiano yao ya ndani labda muwaulize
wenyewe,’’ alisema Wakazi.
Chapisha Maoni