KLABU ya Real Madrid imeifumua mabao 5-0 Athletic Bilbao katika mchezo wa La Liga jana Uwanja wa Bernabeu.
Mwanasoka Bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo amepiga hat-trick ya 22 katika ligi ya Hispania, wakati Mfaransa Karim Benzema amefunga mabao mawili.
Ronaldo alifunga katika dakika ya pili, 55 na 88, wakati Benzema alifunga dakika ya 41 na 69 na sasa Real have imepunguza pengo la pointi dhidi
ya vinara, Barcelona hadi kubaki pointi nne
KIkosi cha Real Madrid kilikuwa: Casillas, Carvajal, Pepe, Ramos/Varane, Marcelo, Modric, Kroos/Illarramendi, Rodriguez, Bale, Benzema/Isco na Ronaldo.
Athletic Bilbao: Iraizoz, Laporte, Benat,
Iturraspe, De Marcos, Susaeta (López
Cabrera), M. Rico, Gurpegi, Muniain/Etxeita, Guillermo/Gomez na Balenziaga.
Chapisha Maoni