0
NAHODHA Wayne Rooney yuko fiti kucheza mechi ya wapinzani wa Jiji la Manchester mwishoni mwa wiki.
Rooney alizua hofu United Jumatatu, wakati alipotolewa nje mazoezini viwanja vya Carrington.
Pamoja na hayo, Nahodha huyo wa United, alifanya mazoezi kikamilifu jana na atacheza dhidi ya Man City Uwanja wa Etihad.Rooney hajacheza tangu mwezi uliopita baada.ya kutumikia adhabu ya mechi tatu kufuatia kadi nyekundu aliyopewa dhidi ya West Ham.
Kocha wa United, Louis van Gaal
amemuambia Rooney wazi ataanza katika mchezo huo, maana yake Robin van Persie ndiye anaweza kuanzia benchi licha ya kufunga bao la kusawazisha dakika za lala salama dhidi ya Chelsea Uwanja wa Old
Trafford Jumapili.

Chapisha Maoni

 
Top