Sata, kilichotokea tarehe 28 Oktoba 2014, mjini London, na kwa kuzingatia Katiba yake Kifungu cha 38 (1) kinachohusu mamlaka ya Rais, kwamba nafasi ya Rais ikiwa wazi kwa sababu yoyote ile, Makamu
wa Rais atakaimu madaraka ya kiti cha
Urais hadi uchaguzi mdogo utakapofanyika ndani ya siku tisini (90), hivyo Serikali imemteua Mhe. Guy Scott (MB), Makamu wa
Rais, kukaimu nafasi hiyo katika kipindi
hiki cha mpito.
Tayari aliyekuwa anakaimu madaraka ya
Urais, Mhe. Edgar Lungu (MB)
ameshamkabidhi madaraka hayo.
Hadi sasa kulingana na taarifa kutoka
Wizara ya Mambo ya Nje, bado
haijafahamika maombolezo rasmi yataanza lini na kwa siku ngapi au mazishi yatafanyika lini. Haya yote yanategemea maamuzi ya kikao cha Baraza la Mawaziri ambacho kinakutana hivi sasa.
Hizi ni taarifa tunazoendelea kupokea,
hivyo nasi tutaendelea kuwataarifu kwa
kadri tunavyozipata.
UBALOZI , LUSAKA , ZAMBIA
Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa
Jakaya Mrisho Kikwete ameshtushwa na
kusononeshwa sana na taarifa za kifo cha Rais wa Jamhuri ya Zambia, Mheshimiwa
Michael Chilufya Sata ambacho
kimetokea jana, Jumanne, Oktoba 28,
2014 kwenye Hospitali ya King Edward
VII, London, Uingereza, ambako alikuwa
anatibiwa akiwa na umri wa miaka 77.
Katika salamu ambazo
amempelekea Makamu wa Rais wa
Zambia, Mheshimiwa Dkt. Guy Scott
kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Rais Kikwete
amesema:
“Nimepokea kwa mshtuko mkubwa
na huzuni nyingi, habari za kusikitisha za kifo cha Mheshimiwa Michael Chilufya Sata, Rais wa Jamhuri ya Zambia. Kwa niaba ya Serikali na Wananchi wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, na hakika, kwa
niaba yangu mwenyewe, napenda
kukutumia wewe Mheshimiwa salamu za
rambirambi za dhati ya moyo wangu, na
kupitia kwako familia ya wafiwa na ndugu wa Hayati Rais Sata pamoja na Serikali na
ndugu zetu wananchi wote wa Zambia
kufuatia msiba huu wa ghafla.”
Ameongeza Rais Kikwete: “Hayati
Sata atakumbukwa daima kama mmoja wa
viongozi wa mfano wa kuigwa katika
Afrika. Katika kipindi chake kifupi cha
uongozi wa juu wa Zambia, alifanikiwa
kuleta mageuzi makubwa katika maisha ya wananchi wengi wa Zambia. Atakumbukwa
pia kwa imani yake isiyoyumba ya
kupigania uhuru, haki na usawa, sifa
ambazo zilimfanya kiongozi mpendwa
ndani na nje ya mipaka ya Jamhuri ya
Zambia.”
Ameongeza Rais Kikwete: “Hivyo,
huyu ni kiongozi ambaye siyo tu
atakumbwa na wananchi wa Zambia lakini atakumbukwa na sisi sote wenzake na
watoto wote wa Afrika.”
“Katika kipindi hiki kigumu cha
majonzi na huzuni, tunaungana nanyi
kuomboleza na kumwomba Mwenyezi
Mungu awape nguvu na subira wana
familia ya wafiwa, jamaa na ndugu zetu
wote wa Zambia ili waweze kuhimili
machungu ya kipindi hiki cha msiba
mkubwa. Aidha, tuko pamoja nanyi katika kumwomba Mwenyezi Mungu aiweke pema roho ya Marehemu Michael Chilufya Sata.”
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
29 Oktoba,2014.
Chapisha Maoni