POLISI mkoani Arusha inawasaka madereva wawili wa magari mawili ambayo yalisababisha ajali iliyoua abiria 12 na kujeruhi wengine watatu.
Madereva hao ni wa basi dogo la abiria aina ya Nissan lenye namba za usajili T519 BDJ na lori la mafuta aina ya Scania lenye namba za usajili T
582 ACR ambao magari yao yaligongana katika barabara ya Arusha Moshi eneo la Madira baada ya basi hilo kutaka kuyapita magari mengine bila
ya kuchukua tahadhari na ndipo likakutana uso kwa uso na lori hilo, hivyo kusababisha ajali iliyoua watu 12, tisa wakifa papo hapo.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, waliokufa na kutambuliwa ni pamoja na Simon Elipokea Ngolenya aliyekuwa kondakta wa basi dogo, Kundaeli Kaaya aliyekuwa mwalimu shule ya msingi Ndoomba wilayani Meru na mkewe, Elly
Kaaya aliyekuwa mtumishi wa halmashauri ya Meru, Idara ya Masjala.
Wengine ni Leticia Ruhangiza ambaye ni Ofisa Elimu ya Watu Wazima katika halmashauri ya Meru na Zakia Kitunga, ambaye ni mwalimu katika
halmashauri ya Meru.
Kamanda Sabas alisema maiti saba bado hawajatambuliwa na wako katika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya mkoa ya Mount
Meru wakisubiri kutambuliwa, kati ya maiti hao saba wanaume wako wanne na wanawake watatu.
Majeruhi ni Alfred Nyabi (36), Mariam Aloyce ambao ni wakazi wa Usa River.
Chapisha Maoni