Ripoti kutoka Vatican inasema ’Kanisa inabidi iwaruhusu na kuwakaribisha wapenzi ambao wapo kwenye mahusiano ya jinsia moja’.
Akizungumza na waandishi wa habari, katika mkutano uliofanyika Oct 13 ambao ulifanyika Jumatatu ili kutoa ripoti hiyo, Kadinali ‘Luis Antonio Tagle wa Philippines alisema ‘Wakatoliki
wanafuatilia sana maswala ya umaskini, vita na uhamiaji na kuacha swala la watu ambao wapo kwenye mahusiano ya kimapenzi ya jinsia moja’.
Lugha hii mpya ya kuhusiana na mapenzi kati ya watu wa jinsia moja inalinganishwa na ‘utetemeko wa Mapasta’, alisema mmoja kati ya waandishi wa habari wa Vatican. ‘Swala la mahusiano ya wapenzi wa jinisia moja linaenda mbali sana mpaka kanisa nalo linajiuliza kama nalo likubali swala hilo bila kuharibu kanuni, sheria na imani
za Kikatoliki’, alisema John Thavis.
Mchungaji James Martin ambae pia ni mwandishi wa neno la Mungu aliiita ripoti hii ya kuhusiana na mahusiano ya wapenzi wa jinsia moja kuwa ni
tendo la “kimapinduzi’, aliendelea kusema kuwa mabadiliko yanayofanywa na kanisa la Kitatoliki kuhusu mahusiano ya wapenzi wa jinsia moja ni
mazuri.
Aliongezea na kusema, ‘watu ambao wapo kwenye mahusiano ya mapenzi ya jinsia moja nao wana uwezo mkubwa wa kuchangia kwenye jamii yetu ya Kikristo’.
Wakatoliki wanaviita vitendo vya mahusiano ya mapenzi ya jinsia moja ‘vitendo visivyo na utaratibu’. Papa Francis, wakati anaongelea swala
la kanisa la Kikatoliki mwaka 2013 alisema ‘mimi ni nani mpaka niwahukumu watu ambao wapo
kwenye mahusiano ya kimapenzi ya jinsia moja?’. Kwa ripoti iliyotolewa jana Oct 13 muhtasari wa wiki nzima kuhusiana mkutano uliofanywa na
karibu Askofu 200, Makardianali na Makuhani pamoja na Papa Francis unaendelea, lakini mpaka sasa hamna mabadiliko yoyote ambayo
yamefanywa.Majadiliano yanaendelea wiki hii na ripoti ya mwisho itatolewa mwisho wa wiki hii.
Chapisha Maoni