Watu watatu wamefariki na wengine sita wakiwa katika hali mbaya Hospitali ya Muhimbili kufuatia tukio la moto uliolipuka kwenye gari la kubeba
mafuta jana maeneo ya Mbagala jijini Dar es Salaam.
Alizumgumza na mwandishi, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu Kamishna Mohammed Mpinga, alisema ajali hiyo haikuleta
athari yoyote baada ya gari lile kupata ajali ila athari ilijitokeza baada ya watu kuvamia na kuanza kuiba mafuta na baadaye kujaribu kuiba betri ndipo cheche za moto zilipolipuka na
kusababisha kuwaka kwa gari hilo.
Wakati huohuo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mecky Sadick, amewataka wananchi kutokuwa na tabia ya kuvamia ama kuiba vitu pindi ajali zitokeapo.
Sadick alisema hayo alipotembelea hospitali ya Muhimbili na Temeke walipolazwa majeruhi hao.
Chapisha Maoni