WACHEZAJI wa sasa na wa zamani wa Ligi Kuu ya England kwa pamoja wameiwezesha Ubelgiji kupata ushindi mnono wa mabao 6-0 dhidi ya Andorra katika mchezo wa Kundi B
kufuzu Euro 2016 mjini Brussels.
Katika mchezo wao wa kwanza wa ushindani tangu watolewe na Argentina katika Robo Fainali ya Kombe la Dunia, Ubelgiji ilipata mabao yake kupitia kwa kiungo wa zamani wa Chelsea, Kevin de Bruyne dakika ya 30 na 34, mshambuliaji wa Tottenham, Nacer Chadli
dakika ya 37, kabla ya Divock Origi, ambaye atajiunga na Liverpool msimu ujao kufunga la nne dakika ya 59 na Dries Mertens kufunga la
tano na la sita dakika za 65 na 68.
Mechi nyingine za Kundi B, Wales ikiongozwa na nyota wa Real Madrid imetoa sare ya 0-0 na Bosnia-Herzegovina wakati Israel
imeifunga Cyprus 2-1.
Chapisha Maoni